Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika (Africa CDC) kilichopo chini ya Umoja wa Afrika (AU) kimeitaka Tanzania kutoa takwimu mpya za mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini humo.
Mkurugenzi wa Africa CDC, Dkt John Nkengasong leo Alhamisi Aprili 14 amesema kuwa kituo chake kwa kutumia takwimu hizo kipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa kuipatia msaada wa kitaalamu na kiufundi unaohitajika.
"Hili ni janga kubwa kwa bara (Afrika) lote na dunia kwa ujumla… hivyo ni kwa faida ya Tanzania kutoa takwimu kwa wakati ili tufahamu mapungufu yapo wapi na tuwasiadie kadri itakavyohitajika," amesema Dkt Nkengasong katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao.
Kwa ujumla wake, Africa CDC imesema inazitaka nchi zote kutoa takwimu kwa haraka kwa kuwa hiko ndicho kiungo muhimu katika kuendesha vita dhidi ya mlipuko wa corona.
Tunaangalia vitu viwili katika takwimu, mosi uharaka wa kutoa taarifa na pili ubora wa takwimu zenyewe."
Dkt Ngasong ametahadharisha kuwa, kwa baadhi ya nchi kuamua kutotoa takwimu kunatengeneza wasiwasi kwa nchi nyengine.
"Katika hili hakuna nchi ambayo ni kisiwa, na virusi havitumii hati ya kusafiria. Endapo nchi X haitatoa takwimu, itatengeneza hali ya wasiwasi kwa nchi nyengine."

Mara ya mwisho kwa Tanzania Bara kutangaza takwimu mpya za corona ilikuwa wiki mbili zilizopita Aprili 29, huku Zanizbar ikitoa takwimu mpya kwa mara ya mwisho wiki moja iliyopita Mei 7.
Mpaka sasa, watu 509 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona nchini Tanzania, huku 183 wakipona na watu 21 kufariki dunia.
Msimamo wa serikali ni upi?
Serikali ya Tanzania inasema kwa sasa kipaumbele chake kipo kwenye uchunguzi wa maabara kuu ya kupima virusi hivyo.
Akizungumza na BBC Swahili jana Jumatano, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt Hassan Abbas amesema: "Tunajiridhisha na vipimo mbalimbali ambavyo vimekuwa vikitumika kwa ajili ya huu ugonjwa…kwa hiyo tunafanya hayo marekebisho."
Dkt Abbas amesisitiza kuwa vipimo kwa wale wenye dalili vinaendelea kufanyika huku marekebisho hayo yakiendelea.
Uchunguzi wa vifaa hivyo unafanyika baada ya rais Magufuli kulitilia shaka ubora wake. Hilo lilitokana na uchunguzi wa siri aliouagiza kwa kutumia sampuli za Wanyama na matunda na baadhi yake kukutwa na virusi.

Maafisa wawili waandamizi wa maabara hiyo wamesimamishwa kazi huku uchunguzi ukifanyika.
Hata hivyo, Africa CDC pamoja na WHO wamesema kwamba vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini Tanzania havina shida yeyote.Kituo hicho cha Africa CDC pamoja na wakfu wa Jack Ma, Shirika la msaada la bilionea wa China, ndio walisambaza vifaa hivyo.
duh
JibuFuta