Ripoti nyingi za unyanyasaji wa nyumbani huwa zinatolewa na wanawake. Theluthi ya wanawake wote na wasichana hupitia unyanyasaji wa kimwili na kingono wakati mmoja katika maisha yao, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.
Ni nadra kwa wenzao wanaume kuzungumziwa kuwa na mashambulio yoyote dhidi ya wanaume wanayofanyiwa na wapenzi wao au watu wa familia.
Unyanyasaji wa nyumbani dhidi ya wanaume ni mwiko kuzungumziwa katika jamii nyingi na mara nyingi, waathirika wa unyanyasaji huo huhangaika na hali zao peke yao.
Mwanaume mmoja kutoka nchini Ukraine aliishirikisha BBC hadithi yake, lakini alitutaka tusitoe utambulisho wake.
Hiki ndicho alichotuambia, pamoja na ushauri wa mtaalamu juu ya jinsi ya kutambua dalili za unyanyasaji wa nyumbani na ni nini unaweza kufanya.
Mwanzoni
Sijui kama rafiki zangu walishuku kitu chochote. Mambo yote yalionekana kuwa ni mazuri nje : sura za tabasamu, marafiki, pesa nyingi, furaha na kujiamini. Tulisafiri nusu ya dunia pamoja.
Sikulazimika kumuogopa wakati tulipokua tukisafiri: Hakuniumiza mbele ya watu. La muhimu lilikua ni kuepuka kuwa wawili mimi na yeye.

Ni hivi karibuni tu nilipogundua kuwa mke wangu wa zamani amekua akinibaka kwa miaka 10.
Ira -alikua ni mke wangu wa kwanza. Tulikutana wakati tulipokua na miaka ishirini na zaidi - yeye ndiye aliyeniomba tuanze kuwa wapenzi.
Wazazi wangu waliniambia ninapaswa kutoka nyumbani kwetu mara moja nikianza mapenzi na mtu yeyote.
Kwa maana nyingine, uhusiano ulimaaninisha kutengana na familia na kuondoka nyumbani katika kipindi cha siku moja nilipoteza kila kitu.
Niliogopa . Kwahiyo niliweza kuwa katika mahusiano tu pale nilipokua na akiba ya kutosha ya pesa za kujikimu kimaisha.
Kutojiamini
Zaidi ya hayo, mama yangu alikuwa hapendi muonekano wangu hivyo alinionea aibu- kwa hiyo sikuwa ninajiamini.
Mara ya kwanza kufanya ngono nililifanya na Ira na wakati huo, niliotaka hilo.
Hatahivyo, haikuwa ya kawaida:Niliumia na nilitumia nguvu. Ngono yetu ya kwanza ilidumu kwa muda wa saa tano, na niliskia maumivu kila mahali baadae.
Alikua na fikra kamba lazima aone majimaji ya mbegu za kiume mwisho wa kitendo. Nilikua nasuguliwa mpaka ayaone. Kwa wastani ngono ilikua inachukua muda wa saa moja hadi saa mbili.
Ngono inapaswa kuwa ni kitu cha kufarahisha, lakini sikuwahi kuifurahia. Sikua na uzoefu na nilikua ninafikiria kuwa hivyo ndivyo inapaswa kuwa,na kwa hiyo nilikua ninamruhusu anipanyie anachotaka.
Lakini baada ya muda mfupi nilikua nikisema"Hapana". Lakini haikumzuia. Hapo ndipo ilipogeuka kuwa ubakaji.

Nilikwama
Ilinibidi niende ng'ambo kwa safari za kibiashara. Nilikua naogopa kumpoteza Ira, kwa hiyo nilikua ninamuomba tunaenda nae. Hata nilikua mtu wa kwanza kumuomba tuoane.
Alikataa, lakini akaishi na mimi. Hapo ndipo matatizo yalipoanzia.
Nilikua nafanyishwa kazi kupita kiasi na nilitaka kupumzika, lakini alidai ngono. Nilikubali mara moja, mara mbili ...alikua anasema, "Ninataka ngono, ninataka, kwahiyo lazima ufanye, hebu njoo, nimekua nikikusubiri kwa muda mrefu ." Nilikua ninamjibu, "Hapana, sitaki, ninataka kupumzika, nimechoka ."
Halafu ananipiga kwa hiyo hakuna chochote ningefanya. Alikua anakwaruza mwili wangu na kucha zake hadi damu inatoka, alikua akinipiga ngumi.
Alikua haniachii alama usoni , alikua anahakikisha ananiumiza sehemu zinazofunikwa na nguo: Kwenye kifua, mgongoni na mikononi.
Sikujibu kwa sababu nilifikiri kumpiga mwanamke ni kumuonea na ni makosa. Hivyo ndivyo wazazi wangu walinifundisha. Nilikua ninajihisi mdogo, dhaifu na sikuweza kukwepa.
Alikua anapata anachokitaka na mara kwa mara alikua juu yangu.

Nilijaribu kukodisha chumba tofauti na yeye wakati mmoja tulipokua hotelini. Lakini sikuwa ninaongea lugha ya mahali hapo, kwa hiyo hawakunielewa katika eneo la mapokezi. Nikaishia kukwama tena katika chumba kimoja na Ira.
Nilikua hata ninaogopa kurudi hotelini baada ya kazi, kwa hiyo ilikua inanibidi nizungukezunguke kwenye maduka kupoteza muda.
Baada ya hayo nilikua ninazunguka mjini. Ilikua ni wakati wa vuli,baridi au mvua, na nilikua nimenunua nguo za baridi.
Kwa hiyo hatimaye nilipata maambukizi ya kibofu cha mkojo(UTI) na homa. Hiyo hata haikumzuia Ira: Nililazimika kufanya anachokitaka.
Siku za wikendi zilikua mbaya zaidi kwamba: Ilitokea Jumamosi asubuhi na Jumapili usiku. Nilianza kuhesabu siku zilizobakia kurudi Ukraine , nilifikiri nitasitisha uhusiano - lakini sikua sahihi.

'Nilijaribu kuondoka katika uhusiano lakini nilikata tamaa'
Nilirudi kwa wazazi wangu na nilikua hata sitaki kuwasiliana tena na Ira, niishi maisha mbali na yeye .
Lakini jaribio langu la kuachana nae lilichukua miaka kadhaa
Tulikua tunapigana, nakata mawasiliano kwa kufunga simu na kujiepusha nae kabisa kimawasiliano. Nilikua ninajificha lakini alikua anakuja na kuketi nje ya mlango.
Alikua ananipigia simu na kuniahidi mambo yote yatakua sawa.
Na nilikua ninarejea kwake kila wakati. Nilikua naogopa kuishi maisha ya upweke.
Mwanzoni , nilijaribu mara nyingi kumuacha, na hatimae nikaamua kukata tamaa. Alisisistiza kwamba tuoane, na tukafanya hivyo, ingawa sikutaka hilo tena.
Ira alikua mwenye wivu kwa kila mtu: marafiki zangu, familia yangu, kila mara aliniita na kuniambia . "Kwani ni lazima nihudhurie hiyo mikutano?" "Kwanini ninakutana na marafiki zangu?" Ilibidi niwe na yeye, au niwe katika eneo analoweza kufika karibu.
Hakuweza kwenda popote bila mimi-Nilikua kitu fulani ambacho kinapaswa kumburudisha wakati wote.

Ira hakuwa na kazi - nilikuwa ninahudumia familia, ninapika na kufanya usafi.
Tulikuwa tumepaga nyumba ya vyumba viwili na mabafu mawili. Nilikatazwa kutumia bafu la chumbani na nilipaswa kutumia bafu la wageni. Kila asubuhi nilikuwa napaswa nisubiri mpaka aamke saa tatu au saa nne au muda wowote atakaojisikia, nilikuwa sipaswi mbughudhi katika usingizi wake.
Aliamua kuwa tunapaswa kulala katika vyumba tofauti na chumba changu kilikuwa hakifungi, hivyo sikuwa peke yangu akijisikia anakuja.
Nilipokuwa nakosea kufanya jambo alikuwa ananipigia kelele na kunipiga, Lazima kila siku alikuwa anipige.
Kitu chochote kibaya kikitokea alikuwa ananilaumu. Nilikuwa namsikiliza anavyosema mwanaume gani anamtaka na nini alikuwa anapaswa kufanya.
Nilikuepo tu sina sauti katika nyumba na nilikuwa nafanya kile ambacho alikuwa anakitaka.
Nakumbuka nilivyokuwa ninakaa kwenye ngazi na kuanza kulia au nilikuwa ninakaa kwenye gari na kuanza kulia. Alikuwa akinikuta nalia ananipita tu kama hajaniona na nikirudi ndani anasema kuwa ananionea huruma.
Hakuna kitu ambacho nilikifanya na kikaonekana kuwa kizuri kwake, hakuna kitu kilichobadilika.
Mimi sio kwamba najua kila kitu au mwema zaidi pia.
Kujizuia kupitia masaibu yote haya nilikuwa naamua kufanya kazi muda mwingi zaidi wakati mwingine nafanya kazi saa 10, 12, 14 kwa siku.
Si jambo rahisi, wengine huwa wanaamua kufanya kazi sana na wengine kunywa pombe tu.

Kwa nini watu wanaonyanyaswa hawawaachi wapenzi wao?

•Watu ambao wamekulia katika familia ambazo kulikuwa na unyanyasaji au wazazi walikuwa wanagombana kila mara.
•Hofu ya kutengwa na kusemwa: "Majirani watasemaje?" "Mtoto anapaswa kulelewa na wazazi wote wawili."
•Hatua ya kwanza -unyanyasaji wa kisaikolojia -ni ngumu kugundua.Hivyo , mtu anayenyanyaswaanakuwa anazoea hali ile taratibu na kushindwa kutafuta namna ya kujikwamua katika hali hiyo.
•Mtu anayenyanyaswa anakuwa hana mahali pa kwenda,anakuwa anamtegemea kifedha mwenza wake anaymnyanyasa au ana ujauzito au watoto wadogo.
•Anapoomba msaada kutoka kwa mamlaka , wanamjibur "Hayo ni matatizo ya kifamilia" na hivyo unakata tama.
Alyona Kryvuliak, kiongozi wa idara ya taifa ya La Strada-Ukraine na Olena Kochemyrovska, mshauri wa taasisi ya Umoja wa mataifa ya mfuko wa idadi ya watu katika kuzuia unyanyasaji wa kijinsia unaosababisha vurugu na matatizo mengi katika jamii.

'Nilianza kuongea na sikuacha'
Wakati upo kwenye hali fulani, unaweza usigundue nini ambacho kinatokea kwako.
Unakuwa huoni namna ya kujikwamua na unakuwa umsikii mtu yeyote. Huoni kama una nafasi ya kutoroka na hakuna matumaini.
Nilikuwa nafanya vitu ambavyo nilikuwa sitaki kuvifanya kwa sababu nilikuwa nimezoea kufanya vitu hivyo sana. Mara zote nilikuwa na deni la kitu kwa wengine na nilikuwa sina ambacho ninakimiliki mwenyewe. Nilijiona mimi ni wa bibi yangu, wazazi wangu na nilidhani kuwa napaswa kujitoa kwa ajili ya wengine kwa sababu ya mahusiano yetu.
Na hivyo nilijitolea maslahi yangu na mimi mwenyewe - wakati huo nilikuwa naona kuwa kila kitu kipo sawa. Hivyo mambo yakawa mabaya zaidi.
Mwanzoni , nilikuwa sipendi lakini ndani ya miaka mitatu mpaka minne ya mahusiano yetu, ngono inaweza kuwa mashambulizi ya hofu. Nilikuwa niahisi hofu kila mara Ira alipokuwa anakutana na mimi kwa nguvu.
Nilikuwa ninahisi wasiwasi, nilikuwa ninamsukuma, ninajificha na kukimbia - nilikuwa ninakimbia nyumbani au kutokuwa chumbani.

Ira alidhani kuwa tuna matatizo ya ngono kwa sababu yangu. Hivyo kila baada ya miaka michache alikuwa ananipeleka kwa mtaalamu wa afya wa masuala ya ngono.
Kila mara niliposema kuwa kuna kitu nilikuwa sikipendi na sikuwa sitaki kujamiiana naye, basi uniambia kuwa nina matatizo.
Hivyo hubaki kimya kwa manyanyaso na kubakwa.
Kwake Ira, kwenda hospitali ilikuwa ni kuhakikisha kuwa yuko sahihi .
Nilizungumzia unyanyasaji wake muda mfupi kabla hatujaachana. Nilianza kuongea na sikuacha.
'Jinsi nilivyopata msaada wa kutoka katika uhusiano huo'
Ilikuwa msimu wa vuli, nilikuwa kitandani ninaumwa kikohozi na homa, joto lilikuwa nyuzijoto 39-40 kwa kipindi cha wiki mbili hivi.
Hakuna mtu ambaye alinijulia hali wakati wote huo. Na nilivyogundua kuwa maisha yangu hayana thamani na hata ningekufa hakuna ambaye angegundua hapo.
Ulikuwa wakati ambao nilipata ufahamu wa kina hata kujionea huruma kwa mateso ambayo ninayapitia. Nilitaka kumwambia mtu lakini nilikuwa sijui nianzaje na nimwambie nani?
Kuna wakati nilienda kwa wazazi wangu nyumbani, lakini sikuwakuta na kujikuta kuwa niko mwenyewe.
Niliangalia kwenye mtandao na kuona matangazo ya kutumiana ujumbe na mtu ambaye simfahamu.
ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kusema kile ambacho kinanipitia. Nilikuwa sijagundua kuwa ule ulikuwa ni unyanyasaji lakini tangu wakati huo nilijifunza kusema 'Hapana' , sitakubali tena.
Mara ya kwanza ilikuwa ni kitu kidogo , kilikuwa ni kitu muhimu kwangu kusema Hapana badala ya kukaa kimya.
Kila nilipokuwa ninahitaji nguvu ,nilikuwa ninakumbuka zile siku ambazo nilikuwa ninaumwa.
Nilipata mtaalamu wa masuala ya familia, ambaye alinipa msaada. Wote Ira na mimi tulikuwa tunaongea tulivyokuwa tunamtembelea mtaalamu huyo na alikatazwa kutonikatisha nnapojieleza. Wakati ambao nilizungumzia kuhusu unyanyasaji.
Alikasirika, alinigombeza na kusema kuwa si kweli.
Hatahivyo alipendekeza tuachane baada ya hapo.Sidhani kama alikuwa anataka hivyo, niliamini kuwa alikuwa anataka kuninyamazisha. Alidhani ni namna ya kunipa nafasi ya kukubal.
Kulikuwa kuna foleni katika ofisi moja, hivyo tukaenda kwa nyingine. Nilikuwa ninajifikiria mwenyewe kuwa bora niamue wakati nina fursa bado na hivyo kukamilisha .

Wakati niliposhika karatasi za talaka yetu, mwezi mmoja baadae, niligundua kuwa siku hiyo ilikuwa siku ya furaha zaidi katika maisha yangu.
Siku kadhaa baada ya talaka, nilimpigia kelele: "Ulikuwa unanibaka!"
" Eh nilikuwa ninakubaka?" alijibu. "Sasa kama nilikubaka?"
Sikuwa na jibu la kumwambia na bado sina. Jinsi alivyokubali kile alichonifanyia na kunicheka nilistaajabu tu.
Nilirudi kuishi kwa wazazi wangu na kupunguza kuwasiliana na Ira. Niliacha kazi yangu na kukaa nyumbani kwa wiki kadhaa, nilihofia kuwa angeweza kuwa anakuja kuniangalia.
Siku moja alikuja tena na kugonga mlango , kupiga mlango kwa mateke na kupiga kelele. Mama aliogopa. Nilitabasamu: "Mama, huwezi kuamini..."
'Ni muhimu kuelewa kuwa inaua'
Sikukusanya ushahidi na sikumwambia yeyote.
Huenda ningewaambia wazazi wangu, lakini tangu utotoni, nilifahamu kuwa hawakuwa na uwezo wa kuficha siri. Sikufahamu pia jinsi ya kuongea na marafiki zangu juu ya mambo ninayoyapitia.
Nilikua natafuta usaidizi kutoka kwa makundi ya Ukraine , lakini yale niliyoyapata yalikua ni ya wanawake pekee.

atimaye,nilipata shirika linalosaidia wanaume kutoka San Francisco.
Mwanasaikolojia wa kwanza niliyemtembelea Ukraine alinicheka : "Mambo hayawi hivyo yeye ni msichana na wewe ni mvulana ." Kwa hiyo nilibadilisha wataalamu wa saikolojia mara sita na hatimae sasa nikapata usaidizi. Ilinichukua miezi minane kabla ya kuruhusu mtu anishike mkono .

Makundi ya usaidizi wa kisaikolojia yaliundwa katika blabu ya akina baba- Fathers' Club community nchini Ukraine, lakini hayakudumu kwa muda mrefu, ni mwanaharakati wa makundi hayo Max Levin anasema.
Kulingana nayeye, wanaume hawakuwa tayari kwenda kwa mwanasaikolojia.
Alyona Kryvuliak kutoka La Strada-Ukraine anasema kwamba wanaume walianza kupiga simu kuomba usaidizi wa wazi wakati La Strada ilipoanzisha namba maalumu ya simu kwa ajili ya wanaume wanaoelezea unyanyasaji wao wa nyumbani inayofanya kazi kwa saa 24.
Wanaume hawakuweza kupiga simu wakati wa saa za kawaida za kazi.
Lakini hata sasa, wanaume wanahofia kufahamika na hawako tayari kutetea haki zao katika taasisi za umma, kama vile mahakamani na kwa maafisa wa usalama.
kwa waathiriwa wa unyanyasaji wanaume, kujinasua kisaikolojia katika mtego wa unyanyasaji unaweza kuwa mchakato mrefu, anaelezea tatizo mwanasaikolojia Yulia Klymenko. Kwanza kabisa jamii haimsaidii mwanaume kwa kauli mfano "wanaume hawalii" au "wanaume wana nguvu ".
Mtu mwenye unyanyasaji wa kingono, kisaikolojia au kimwili huwa anaonekana kama mtu asiye wa kawaida katika jamii . Kwa mujibu wa Bi Klymenko, wateja wenye matatizo haya makubwa tofauti wanahitaji msaada bila kujali ni wa jinsia au umri gani.
Ninaangalia uwezekano wa kumpeleka mahakamani. Mawakili walisema kuna uwezekano wa kupata amri ya kumzuwia kuishi name. Lakini sasa siihitaji. Kwa muda mrefu, nimemua nikitaka tu akiri kile alichonifanyia na aniombe msamaha.

Bado siendi kazini na inaniwia vigumu kwangu kutoka kitandani kila siku. Sina la kujivunia maishani. Sijui hata nimekua nikifanya nini miaka yote hii.
Ninachokifahamu ni kwamba sitakua tena na uhusiano wa kimapenzi na sitakua na watoto. Nimekata tamaa.
Lakini la kusikitisha nimekua kimya kwa muda mrefu, na imesababisha matatizo makubwa!
Labda kuna mwanaume anayepitia hali kama yangu sasa hivi na atasoma simulizi yangu,
Ni muhimu kuelewa: Haitaisha, haiwezi kutatuliwa, ni tatizo halisi ambalo haliwezi kuisha na litakuua. Kama unaelewa haya basi una fursa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni