MLM Gateway - Helping network marketers build their business

TANZIA: Babu Njenje afariki dunia


mwanamuziki mkongwe wa Bendi ya Kilimanjaro maarufu kama Wana-Njenje, Mabrouk Hamis Omar almaarufu kama Babu Njenje amefariki dunia leo jijini Dar baada ya kuugua kwa muda mrefu.










Marehemu Babu Njenje ambaye alizaliwa mwaka 1947 Wilayani Pangani, Tanga,alianza kazi ya Muziki wakati anasoma shule ya Usagara Sekondari Mkoani Tanga, na baadaye akajiunga na Band ya Love Burg huko Tanga, kisha Marehemu alijunga na Band ya Revolution na ilipofika mwaka 1989 yeye pamoja na wanamuziki wenzake akiwemo Abdallah Dulla,Hemed Salim Chuki, Babu Njenje, Mohamed Mrisho, Waziri Ally pamoja Keppy Kiombile walianzisha The Kilimanjaro Band.


Share:

Diamond Platnumz ,WCB watoa wimbo wa pamoja ‘Quarantine’






Lebo ya muziki wa Bongo Fleva WCB Wasafi imeungana na kutoa wimbo mmoja wa  ‘Quarantine’ ambapo wamo Diamond Platnumz, Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Zuchu na Queen darlin.






https://youtu.be/wwf09xtoQHU

Share:

“Nilichokiona ni moto tu”-Manusura ajali ya Ndege Pakistan asimulia.


Mmoja wa watu walionusurika ajali ya ndege siku ya Ijumaa nchini Pakistani katika mji wa Karachi aelezea kuhusu tukio hilo ambalo analiona kama ndoto ya kutisha, anasema alikuwa anaona moto tu.









Abiria wa ndege ya Pakistan Muhammad Zubair ni miongoni mwa abiria wawili ambao walinusurika katika ajali hiyo ya ndege ya kimataifa ya ‘Pakistan International Airlines (PIA) Airbus A320’ iliyoanguka katika makazi ya watu.





Mamlaka ya afya katika jimbo la Sindh imesema kuwa vifo 97 vimethibitishwa .





Chanzo cha ajali kikiwa hakijafahamika bado.





Rubani aliripoti tatizo la kiufundi baada ya jaribio la kwanza la kutua kushindwa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo kisha akapiga simu wakati ndege inaanguka.









Ajali hii imetokea siku chache tu baada ya mamlaka ya Pakistan kuruhusu ndege za biashara kuanza shughuli zake baada ya kulegeza masharti kutokana na hatua ya kutotoka nje kuzuia maambukizi ya corona.





Muhammad Zubair aliwezaje kupona ajali hiyo?





Ndege namba PK8303, Airbus A320 ambayo ilikuwa na abiria 91 na wafanyakazi wanane wa ndege hiyo – ilikuwa na familia nyingi ambazo zilikuwa zinasafiri kwa ajili ya mapumziko ya sherehe za Eid siku ya Jumapili – walikuwa wanasafiri kutoka Lahore.





Ndege hiyo ilikuwa inajaribu kutua uwanja wa kimataifa wa Jinnah uliopo mjini Karachi majira ya saa nane na nusu saa za taifa hilo wakati ilipoanguka.





Bwana Zubair, ambaye alipata majeraha kidogo anasema ndege ilikuwa inataka kushuka katika uwanja wa ndege lakini ikashindwa na kupata ajali dakika 10-15 baadae.





“Hakuna ambaye alifahamu kuwa ndege ilikuwa inaenda kuanguka, safari ilikuwa nzuri tu na hatukuhisi utofauti wowote,” alisema.





Nilipoteza fahamu baada ya ajali, “Wakati ambao nimezinduka nilisikia tu kelele za watoto na watu wazima kila kona. Nilichokiona ni moto tu. Nilikuwa sioni mtu yeyote zaidi ya kelele nyingi za vilio “.





” Nilifungua mkanda wa kiti changu na kuona mwanga – nikaanza kufuata mwanga na ilinibidi niruke kama mita 3 (futi 10) ili kuwa salama”, aliongeza.





Map of Pakistan highlighting Lahore and Karachi




Ajali iliyokea eneo la makazi




Kwa nini ndege hiyo ilianguka?





Ndege ilikuwa karibu na usawa wa makazi ya watu wakati ilipogonga majengo yaliyojengwa wakati wa ukoloni.





Picha za video zinaonyesha jinsi kikosi cha uokoaji kilivyokuwa kinajaribu kuokoa watu waliokuwa katika eneo hilo.





Magari kadhaa yalishika moto pia.





Shahidi wa tukio hilo Mohammed Uzair Khan ameliambia shirika la BBC kuwa alisikia sauti za watu wengi nje ya nyumba yake.





“Karibu nyumba nne ziliharibiwa kabisa, kulikuwa na moto mkubwa na moshi mwingi,” alisema. “Walikuwa majirani zangu, siwezi kuelezea tukio lilikuwa baya kiasi gani?”





Mawasiliano kati ya mwongozaji ndege na rubani yalichapishwa katika vyombo vya habari vya Pakistani. Rubani alisikika akisema ndege ilikuwa inahitilafu katika ‘injini”.





Mwongozaji wa ndege alikuwa anamuuliza rubani kama anaweza kuendelea kuishusha ndege hiyo”, na rubani alikuwa anajibu kwa ishara kuwa bado kuna shida.









Maofisa wa masuala ya anga wameiambia Reuters kuwa ndege hiyo ilishindwa kufuata uelekeo wake.





Picha ziliwekwa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa ndege ilikuwa inatatizo kwenye injini zake zote na isingeweza kufika katika eneo ambalo lilikusudiwa.





Wachunguzi watajaribu kuona nini ambacho kipo katika kisanduku cha sauti cha kwenye ndege ‘black box’ ili waweze kubaini chanzo cha ajali hiyo.





Kamati ya uchunguzi wa ajali hiyo tayari imepangwa.





Ndege hiyo ambayo ilianza kufanya kazi mwaka 2014 na ilifanyiwa ukaguzi mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka jana.





rescue workers search the wreckage
Ndege ilianguka katika makazi ya watu




Tunafahamu nini kuhusu watu waliofariki katika ajali hiyo?





Kwa mujibu wa mamlaka ya nchi hiyo, vifo 97 vimethibitishwa ingawa haijawekwa wazi katika idadi hiyo wangapi ni abiria wa ndege na wangapi ni wakazi wa eneo hilo.





Maiti 19 ziliweza kufahamika.





Rais wa benki ya Punjab, Zafar Masud, ni miongoni mwa watu walionusurika katika ajali hiyo, alisema msemaji wa serikali.





Mwandishi wa habari wa chaneli ya TV ya 24 News, Ansar Naqvi, na aliyekuwa meneja wa mamlaka wa majanga wa Punjab, Khalid Sherdil, walikuwa katika orodha hiyo ya abiria ambao labda wamenusurika.





relative of one of the victims mourns
Wengi waliokuwa wanassafiri ni familia zilizokuwa zinaenda kusherehekea sikukuu ya Eid




Jumamosi ibada ya mwisho kwa baadhi ya waathirika ilifanyikamjini Karachi. Vipimo vya vinasaba vinafanyika kubaini miili ya wengine kabla ya kukabidhiwa familia zao.





Waziri mkuu wa Pakistan, Imran Khan alisema alishtuka na kusikitishw ana ajali hiyo na kuahidi kufanyika kwa uchunguzi haraka iwezekanavyo.





Lakini Chama cha Shirika la Ndege la Pakistan kimesema hakina imani na uchunguzi huo na kimeita wachunguzi wa kimataifa kujuika katika jopo la uchunguzi wa ajali.





Rekodi ya usalama wa anga Pakistan inasema?





Licha ya kwamba mamlaka ya anga inajisifu katika utendaji wake, lakini historia ya ajali za ndege iko hivi nchini Pakistani;





Mwaka 2010,ndege binafsi ya Airblue ilipata ajali karibu na Islamabad, na kuua watu wote kwenye ndege ambao walikuwa 152 – hii ni ajali mbali Zaidi kutokea nchini Pakistan.





Mwaka 2012, ndege aina ya Boeing 737-200 ambayo ilikuwa inafanya safari zake Pakistan- Bhoja Air ilipata ajali mbaya ikiwa inakaribia kutua Rawalpindi,na kuuwa abiria wote 121 na wahudumu wa ndege sita.





Na mwaka 2016, ndege ya kimataifa ya Pakistan ililipuka wakati ilikiwa inaelekea magharibi mwa Pakistan kuelekea Islamabad, na kuua watu 47.


Share:

Watu milioni 5 waambukizwa Corona kote duniani


Idadi ya watu ambao wameambukizwa virusi vya Corona kote duniani imezidi milioni 5, latin Amerika ikiongoza kwa maambukizi ya kila siku kuanzia wiki iliyopita, ikifuatiwa na Marekani Pamoja na Ulaya.

Maambukizi yanaonyesha awamu mpya ya kusambaa kwa virusi hivyo, ambayo yalifikia kilele chake mwezi Februari nchini China, kabla ya kuongezeka Ulaya na Marekani.

Latin Amerika imeripoti robo tatu ya maambukizi ya watu 91,000 yaliyoripotiwa wiki iliyopita.

Ulaya na Marekani zimerekodi asilimia 20 ya maambukizi kila mmoja.

Idadi kubwa ya maambukizi imeripotiwa nchini Brazil, ambayo karibuni iliripoti maambukizi ya watu wengi kuliko Ujerumani, Ufaransa na Uingereza


Brazil ni ya tatu duniani kuripoti idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya Marekani na Russia.

Maambukizi yanaongezeka sana nchini Brazil kila siku na kuiweka nchi hiyo katika nafasi ya pili baada ya Marekani.

Watu 326,000 wamefariki kutokana na maambukizi ya Corona kote duniani. Zaidi ya nusu ya idadi ya vifo imeripotiwa Ulaya.

source: VOA


Share:

SERIKALI YATOA RIPOTI YA UCHUNGUZI WA MAABARA YA TAIFA YA AFYA YA JAMII


Serikali imetoa ripoti ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii iliyoko ofisi za Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadam (NIMR) jijini Dar es Salaam na kubaini mapungufu mbalimbali ya kiutendaji yaliyokuwepo katika maabara hiyo.

Akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametaja mapungufu yaliyobainishwa na kamati hiyo kuwa moja kati ya mashine za kupima sampuli za COVID-19 ilikuwa na hitilafu bila uongozi wa maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo.

Taarifa hiyo pia imebaini kuwepo kwa upungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19. 

Waziri Ummy amesema kamati hiyo pia imetaja kuwepo kwa upungufu wa wataalamu wenye sifa za mafunzo ya “Biotechnology & molecular Biology” katika sekta ya Afya ikiwemo katika Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii.

Kufuatia taarifa ya kamati ya uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii kuhusu upimaji wa sampuli za ugonjwa wa COVID- 19, Wizara ya Afya imechukua hatua ya kuhamisha shughuli za upimaji wa COVID – 19 kutoka kwenye maabara iliyoko NIMR na  kuanza kutumika kwa mashine nyingine za maabara mpya iliyopo Mabibo, Dar es salaam.

“Kuanzia sasa shughuli zote za upimaji wa maabara ya taifa ya afya  ya  jamii zitafanyika katika maabara mpya ya mabibo yenye vifaa vya kisasa vyenye ubora na uwezo wa kupima sampuli 1,800 ndani ya masaa 24” amesisitiza Waziri Ummy.

Amesema maabara iliyokuwa inatumika awali na kukutwa na mapungufu ilikuwa na uwezo wa kupima sampuli 300 kwa masaa 24 na ilianzishwa mwaka 1968 katika ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadam (NIMR), mtaa wa Obama kati kati ya jiji la Dar es Salaam zitaendelea kupima magonjwa mengine.

“hivi sasa Upimaji wa Sampuli zote za COVID-19 umehamishiwa kwenye Maabara hii ya Mabibo, Dar es Salaam ambayo kuanzia sasa ndiyo itakuwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii. Maabara hii ambayo ujenzi wake umekamilika mwezi huu ina miundombinu inayojitosheleza, mashine za kisasa zinazoweza kupima sampuli nyingi na kutoa majibu ya uhakika na kwa haraka” amesema Waziri Ummy.

Aidha, Wizara imeshaandaa wataalam zaidi wenye sifa na vigezo kwa ajili ya Maabara hiyo na imeanza kurekebisha mfumo wa utawala, utendaji na kitaaluma ndani ya Maabara ya Taifa.

Waziri Ummy Mwalimu aliunda Kamati ya wataalam iliyoanza kazi rasmi tarehe 6, Mei, 2020 ya kuchunguza mwenendo wa maabara ya taifa ya afya ya jamii ikiwa ni pamoja na kuangalia mfumo mzima wa ukusanyaji na upimaji wa sampuli za COVID – 19.

Kamati hiyo iliundwa kufuatia mashaka yaliyoelezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli kuhusu usahihi wa vipimo vya COVID – 1.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi ametoa mwongozo wa kusaidia jamii kushiriki katika ibada ya shukrani na sala ya Eid El Fitr kwa hali ya usalama ili kuepusha kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Prof. Makubi amewataka  wananchi kuchukua tahadhari katika siku tatu ambazo nchi itaingia katika maombi maalum ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kupungua kwa maambukizi ya virusi ugonjwa wa Corona.

“ ni muhimu wananchi wakasherehekea salama kwa kuchukuwa  tahadhari kwani ugonjwa huo bado upo” Amesisitiza Mganga Mkuu wa Serikali.

Katika kufanikisha uwepo wa mazingira salama wakati wa shukrani na sala ,Viongozi wa Mitaa, Viongozi wa Afya na uongozi wa maeneo yote ya Ibada na misikitini wanapaswa kuhakikisha uwepo wa vifaa vya kunawia mikono, maji tiririka na sabuni au vitakasa mikono kwa ajili ya usafi binafsi wa waumini wote katika maeneo ya kuingilia .

Aidha, Prof. Makubi ameshauri sehemu za kufanyia ibada ziwe na nafasi ya viti kupangwa zaidi ya mita moja kwa wale wanaokaa au kusimama na wananchi wote wanapokwenda kushiriki au kutembelea maeneo ya Ibada/Sala wanashauriwa watumie barakoa za vitambaa ambazo kwa sasa zipo kwa wingi na zinatengenezwa hapa nchini na wananchi wenyewe.

Amewataka wananchi kuepuka mikusanyiko na kuhakikisha wanakaa umbali usipoungua mita moja kati ya mtu na mtu wakati wote wa shukrani na wakati wa shukrani waendesha ibada/sala wawakumbushe wananchi mara kwa mara kuzingatia taratibu za kujikinga na maambukizi kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya

Mganga Mkuu wa Serikali amewakumbusha Wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma kuzingatia maagizo ya Serikali ya kutosimamisha abiria kwenye mabasi, na vilevile wahudumu wote wawe wamevaa barakoa za vitambaa.









 


Share:

Hatuwezi kuendelea kukaa tu nyumbani- Uhuru Kenyatta


Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya




Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mipango ya kusaidia biashara na raia kusonga mbele katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi kwasababu ya janga la virusi vya corona





Rais amehutubia taifa kutoka Ikulu ya rais, Nairobi na kusema kwamba mipango hiyo itagharimu shilingi bilioni 53.7.





Katika hotuba yake, rais alisema pesa hizo zitagawanywa katika sekta muhimu kama vile miundo mbinu, elimu, biashara ndogo ndogo na za wastani, afya, kilimo, utalii, mazingira na viwanda vya uzalishaji.





Aidha, rais amesema kuwa taifa hilo haliwezi kuendelea kuchukua hatua za kusalia ndani milele.





''Sisi kama serikali, kama serikali zingine, mataifa yote dunia zimeanza kuona, hatuwezi kuendelea kusema wakenya tukae nyumbani, hatuwezi kuendelea kusema tu wakenya msiende kufanya biashara, musiende makazi, namna hio. Lakini, ile kitu ambayo itatusaidia pia kwa kikamilifu kuhakikisha ya kwamba tumeweza tena kufungua uchumi wetu na wananchi waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida. Nimewaambia wenzangu, hii haitakuwa kwa sababu ya yale serikali itatenda, itakuwa kwa sababu ya yale kila mmoja wetu kwa kibinafsi atafanya''.





Kenya inachukua hatua sawa na zile ambazo pia zimechukuliwa na nchi nyengine kama hatua ya kuchechemua uchumi unaoendelea kudidimia.





Uhuru amesema hayo wakati ambapo pia alitangaza kuwa Kenya maambukizi 31 ya virusi vya corona na kufikisha idadi hiyo hadi 1192.





"Hadi kufikia sasa tumepima watu 57,640 ambapo 1192 wamethibitishwa kuambukizwa na wengine karibia 50 wakipoteza maisha yao kwasababu ya ugonjwa huu,'' rais alisema.





''Mimi sina shaka Wakenya tukishirikiana, tuungane pamoja, tutashinda huu ugonjwa. Lakini tena leo wakati natoa hii hotuba ambayo tumetoa sasa ya kusema lengo mbali mbali ambayo serikali inachukua kurahisisha maisha ya wananchi wa kawaida na kuhakikisha ya kwamba wananchi bado wanaweza kuendelea na maisha yao kupitia hio stimulus package ambayo nimeitaja, lazima tukumbuke ya kwamba jukumu ni letu sisi sote''.





Alieleza raia wa Kenya kwamba ikiwa wataendelea kutekeleza masharti yaliyowekwa bila shaka taifa hilo litafanikiwa kukabiliana na changamoto zilizopo kwa sasa.





Kama hatua moja ya kuhakikisha usalama wa kila mmoja, wadau mbalimbali ikiwemo mawaziri na maafisa wa afya, wameagizwa kuanza kuwaeleza wakenya kwamba hawatasalia ndani milele.





Rais aliendelea kusihi raia kuwa kila mmoja anajukumu la kuhakikisha usalama wake na wengine.





''Wewe uko na jukumu la kuhakikisha umechunga mwenzako, tukianza kupanua na kufungua uchumi wetu, wewe ujue ya kwamba, usipotii masharti ambayo tumepatiwa, sio wewe pekee yako utaumia, unaumiza pia mwenzako kwa kazi ambayo unafanya. Ukienda nyumbani umeumiza mama, umeumiza mtoto''.





''Itafika wakati tutafungua taifa letu na wakati wa kufungua, jukumu sasa itarudi kwako, itarudi kwangu kibinafsi. Kuhakikisha ya kwamba umejilinda, umelinda wale unapenda, na unalinda wale mnafanya kazi pamoja na wao''.





Rais Uhuru Kenyatta ameonyesha kwamba njia moja ya kukabiliana na changamoto hii kwa muda mfupi, nchi hiyo inapanga kurekebisha barabara na miundo mbinu mingine.





Aliongeza kwamba bilioni 5 zimetengwa kwa ajili ya wenyeji kupata ajira zitakazoibuka katika utekelezaji wa mipango hiyo.





Pia serikali imetoa bilioni 6.5 kwa Wizara ya Elimu kuajiri waalimu zaidi 10,000 huku akitangaza kuwa serikali itanunua magari yaliyotengenezwa ndani ya nchi hiyo kiasi cha milioni 600 kukuza viwanda vya utengenezaji magari nchini humo.





Aprili mwaka huu, rais Uhuru Kenyatta alitangaza kusitishwa kwa shughuli za usafiri katika kauni za Nairobi, Kilifi, Kwale na Mombasa. Hatua nyengine iliyochukuliwa ni kusalia ndani kuanzia saa moja usiku hadi kumo na moja asubuhi.





Rais amesema asilimia 82 ya ugonjwa wa Covid-19 ni kutoka Nairobi huku kaunti zingine za Mombasa zikirekodi asilimia 14.






Share:

Habari za Magazeti ya Tanzania leo May 24, 2020


Karibu tena mtanzania mwenzangu,siku ya leo May 24, 2020,karibu tutazame kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.


















































Share:

Habari za Magazeti ya Tanzania leo May 23, 2020


Leo ni May 23, 2020,nakukaribisha mtanzania mwenzangu kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.


































































Share:

Barcelona wamepunguza bei ya kumuuza beki wao wa kati Samuel Umtiti


Barcelona wamepunguza bei ya kumuuza beki wao wa kati Samuel Umtiti, 26, mpaka kufikia pauni milioni 27 tu, wakati huu ambapo klabu za Manchester United na Arsenal zinamnyatia mchezaji huyo. (Sport - in Spanish)





Man United wameazimia kuwa kusajili beki mpya wa kati kuwa ni suala la kipaumbele kwa dirisha lijalo la usajili huku kocha Ole Gunnar Solskjaer akiamini sasa ana nafasi nzuri Zaidi ya kumnasa beki wa Napoli na Senegali Kalidou Koulibaly, kwa kuwa PSG imeacha kumfuatilia. (Express)





Dortmund players observed social distancing protocol as they celebrated Haaland's goal
Wachezaji wa Dortmund wakizingatia hatua ya kutokaribiana wakati wanafurahi kupata goli




Real Madrid na Manchester United huenda wakatakiwa kusubiri mpaka miaka miwili ijayo ili kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland, 19, kwa kuwa mkataba wake wenye kifungu cha bei cha dola milioni 75 unasema anaweza kuuzwa kuanzia 2022 na si chini ya hapo. (Evening Standard)





Kiungo wa Juventus na Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 30, anatarajiwa kukataa kuhamia Ligi ya Primia mwishoni mwa msimu, huku Cchelsea ikitajwa kama moja ya klabu ambazo ilikuwa ikimtolea macho. (Mundo Deportivo - in Spanish)





Arsenal wanapanga kufanya usajili wa pauni milioni 25 kumnasa beki wa Dortmund na Uswizi Manuel Akanji, 24, baada ya kuwa katika mazungumzo naye toka mwezi Januari. (Sun)





Adrien Rabiot
Adrien Rabiot kiungo wa Juventus na Ufanransa




Wakati huohuo, washika bunduki hao wa London wamejiunga na Everton katika mbio za kumsajili kiungo wa Juventus na Ufanransa Adrien Rabiot, 25, huku wakiamini kuwa wakimpata atapata ushirikiano mzuri na mfaransa mwenzake Matteo Guendouzi, 21. (Le10 Sport - in French)





Paris St-Germain bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, ambaye amesalia na mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa na Arsenal. (Le10 Sport - in French)





Celtic's Kristoffer Ajer tips the ball past team mate Jack Hendry and Alashkert's Artak Grigoryan
Kristoffer Ajer (kulia)




Klabu za Leicester, Manchester City, Wolverhampton Wanderers na Everton zinamnyatia beki wa Celtic na Norway Kristoffer Ajer, 22. (90min.com)





Kiungo wa Dortmund na Ujerumani Germany Emre Can, 26, amesema hawezi kujiunga na Manchester United kwasababu "moyo wangu hauwezi kukubali" baada ya kuchezea klabu ya Liverpool. (Bild, via Mirror)


Share:

Marekani kuipa Tanzania Bilioni 5.6 za ziada kusaidia kupambana na corona


Marekani imetangaza kuwa kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) itaongeza kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 2.4 (Takriban Shilingi za Kitanzania bilioni 5.6), ikiwa ni msaada kwa sekta ya afya nchini Tanzania ambapo msaada huu unalenga kuimarisha uwezo wa maabara na upimaji wa kimaabara, kusaidia jitihada za utoaji taarifa, miradi ya maji na usafi wa mazingira, kuzuia na kudhibiti maambukizi, kutoa elimu ya afya kwa umma na miradi mingine.





Fedha hizi ni nyongeza ya msaada wa Dola za Kimarekani milioni 1 unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya janga la COVID-19 uliotolewa hivi karibuni na kufanya kiasi kipya cha fedha zilizotolewa kwa Tanzania ili kukabiliana na janga hili kufikia Dola za Kimarekani milioni 3.4. 





Isitoshe, kiasi kingine cha Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimebadilishwa matumizi na kuelekezwa kwenye mapambano dhidi ya janga hili. 





Hii inafanya jumla ya fedha zote zilizotolewa na Marekani katika kukabiliana na COVID-19 nchini Tanzania hadi hivi sasa kufikia Dola za Kimarekani milioni 5.3 (Sawa na Shilingi za Kitanzania bilioni 12.2).
Taarifa hiyo imeongea kuwa katika kipindi cha miaka 20 iliyopita Marekani imewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 7.5 kwa maendeleo ya Tanzania huku karibu Dola za Kimarekani bilioni 4.9 zikielekezwa kwenye sekta ya afya pekee ambapo toka mwaka 2009 Serikali ya Marekani imetoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 100 kusaidia miradi ya afya na takriban Dola za Kimarekani bilioni 70 kama msaada wa kibinadamu duniani kote.
Imeeleza pia kuwa, Serikali ya Marekani inaendelea kuwa mfadhili mkubwa zaidi duniani wa miradi ya afya na shughuli za kibinadamu zinazolenga maendeleo ya muda mrefu na jitihada za washirika wake kujijengea uwezo na kuchukua hatua za dharura wakati wa majanga. Aidha tunaongoza duniani katika utoaji wa misaada ya kibinadamu na kiafya katika kukabiliana na janga la COVID-19.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Marekani inaendelea kuonyesha uongozi katika jitihada za kimataifa za kukabiliana na janga la COVID-19, Watu wa Marekani wametoa zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 10 zitakazosaidia jitihada za kimataifa za kukabiliana na COVID-19 






Share:

Taarifa Kwa Umma Kutoka Jeshi La Polisi Tanzania











Share:

Waziri Ndalichako: "Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29 Juni, 2020"


Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako amesema Mitihani ya Kidato cha 6 itaanza Juni 29, na kumalizika Julai 16, 2020.

Amesema  mitihani hiyo itaenda sambamba na ile ya Ualimu na kulitaka Baraza la Mitihani kuhakikisha wanasambaza ratiba inayoonesha mitihani itakavyofanyika.


Ndalichako ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa May 22 wakati akiongea na Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli aliyoyatoa jana.

"Wanafunzi wa kidato cha sita watafungua tarehe 01/06/2020  kama ilivyoelekezwa na Rais Magufuli na wanafunzi watakuwepo shuleni wakijisomea na kufanya maandalizi ya mitihani mpaka tarehe 28/06/2020


"Mitihani ya kidato cha sita itaanza rasmi tarehe 29/06/2020 na itafanyika hadi tarehe 16 Julai 2020, mitihani hiyo ya kidato cha sita itaenda sambamba na mitihani ya ualimu





"Tumeliagiza Baraza la Mitihani la Tanzania kuhakikisha kwamba mitihani hii inapokamilika, ni lazima matokeo yake yatoke kabla ya Tarehe 31 Agosti,2020, ili tuweze kuendana na maelekezo ya Mhe. Rais kwamba wanafunzi hawa waweze kujiunga na vyuo vikuu "- Amesema Waziri Prof.Ndalichako.


Share:

“Hakuna Beef Na Lady Jaydee”- Meneja wa Ally Kiba


Meneja wa msanii wa Bongo Fleva Ali kiba ameweka wazi kuwa hakuna ugomvi wowote baina ya msaani huyo na Lady Jaydee





Kauli ya meneja huyo inakuja kutokana na majibu ya Lady Jaydee alipoulizwa na shabiki mmoja kwenye mtandao wa twitter iwapo itafanya collabo na Ally Kiba





“Jay dee ni msaanii tunaye mheshimu ni dada na sidhani kama kuna ugomvi wowote baina yake yeye na Kiba maan tumeshirikiana mara nyingi kipindi akiwa Rockstar (label ya Ali kiba) labda kama kuna shida nyingine ila sisi hatuna shida” amesema Aidan Charlie alipoulizwa na clouds Tv





Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Ally Kiba kushirikiana ilikuwa mwaka 2012 walipotoa wimbo wa Single Boy wa Ali Kiba, Jay Dee alipoulizwa kama atafanya collabo na mkali huyo alisema hana mpango na afikirii leo wala kesho


Share:

Gloomy Sunday, Wimbo Uliosababisha Watu zaidi ya 100 Kujiua


Gloomy Sunday (Jumapili ya Huzuni) ni wimbo uliotungwa na Rezso Seress (Rudi Spitzer), msanii kutoka nchini Hungary mwaka 1933. Reszo alitunga maneno ya wimbo huo na kupiga mwenyewe ala ya huzuni ya wimbo huo, baada ya kuachwa na mpenzi wake.





Inaelezwa kwamba kitendo cha kuachwa na mwanamke aliyekuwa akimpenda sana, kilimfanya apatwe na huzuni kali na msongo wa mawazo, na katika kipindi hicho ndipo alipopata wazo la kutunga mashairi na baadaye kuutengeneza wimbo huo.





Kwa sababu aliuimba akiwa na huzuni kali, wimbo nao ulijawa na hisia kali, za mtu anayelalamika kuvunjwa moyo na mpenzi wake, akifananisha kitendo cha kuachwa kuwa sawa na kufiwa na mpenzi aliyekuwa anampenda.





Awali ulionekana kuwa wimbo wa kawaida wa huzuni, lakini matukio ya watu kuyakatisha maisha yao baada ya kuusikiliza mara nyingi wimbo huo kwa kuurudiarudia yalianza kuripotiwa, wengine wakiacha kabisa ujumbe kwamba wamejiua baada ya kusikiliza wimbo huo.





Miaka miwili baadaye, serikali ya Hungary iliupiga marufuku wimbo huo, hata hivyo tayari ulikuwa umesambaa sana, kiasi kwamba watu bado waliendelea kuusikiliza, hasa pale inapotokea mtu ameachwa au ameumizwa na ampendaye.





Sifa za wimbo huo zilianza kusambaa duniani kote na mwaka 1936, wanamuziki wa Marekani na Uingereza waliutafsiri wimbo huo kwa lugha ya Kiingereza, kutoka lugha ya awali ya Ki-hungary, bado tatizo lilelile likawa linaendelea hata kwa matoleo yaliyotafsiriwa, watu wakawa wanaendelea kujiua baada ya kuusikiliza.





Mwanzoni mwa miaka ya 1940, toleo la Kiingereza la wimbo huo lilipigwa marufuku nchini Uingereza baada ya idadi ya waliokuwa wakijiua kuzidi kuongezeka lakini Marekani na sehemu nyingine duniani wimbo huo uliendelea kupigwa





Miaka michache baada ya wimbo huo kumpatia mafanikio makubwa na kuwa gumzo dunia nzima, Seress aliamua kumtafuta mwanamke aliyemuacha na kusababisha atunge wimbo huo, lengo lake likiwa ni kujaribu kumbembeleza ili warudiane kwani kama ni pesa, tayari alikuwa nazo baada ya wimbo huo kuwa maarufu dunia nzima.





Hata hivyo, katika hali ya kustaajabisha, inaelezwa kwamba Seress alipofika mahali alipokuwa akiishi mwanamke huyo, alikuta watu wamejaa, baadaye ikabainika kwamba mwanamke huyo amekunywa sumu na kujiua na kwenye chumba alichojiulia, ilibainika kwamba alikuwa akisikiliza wimbo huo na pia aliacha ujumbe wenye maneno mawili, kama sababu za kujiua kwake; Gloomy Sunday.





Inaelezwa kwamba Seress alibaki na hatia kubwa ndani ya moyo wake, akiamini kwamba yeye ndiyo chanzo cha kifo cha mwanamke huyo na mwaka 1968, naye aliamua kuyakatisha maisha yake kwa kujirusha ghorofani kupitia dirisha la chumba alichokuwa akiishi, nchini Budapest.





Seress aliacha ujumbe kwamba ameamua kuyakatisha maisha yake baada ya kuona wimbo alioutunga, umekuwa sababu za watu wengi kujiua hivyo anahisi hatia kubwa ndan ya moto wake, akawaomba radhi ndugu na marafiki wa wote waliojiua kwa sababu ya kusikiliza wimbo huo.





Lyrics (Literal Translation)
On a sad Sunday with a hundred white flowers
I was waiting for you, my dear, with a church prayer
That dream-chasing Sunday morning
The chariot of my sadness returned without you.
Ever since then, Sundays are always sad
Tears are my drink, and sorrow is my bread.
Sad Sunday. Last Sunday, my dear, please come along,
There will even be priest, coffin, catafalque, hearse-cloth.
Even then flowers will be awaiting you, flowers and coffin.
Under blossoming (flowering in Hungarian) trees
My journey shall be the last.
My eyes will be open, so that I can see you one more time
Do not be afraid of my eyes as I am blessing you even in my death.
Last Sunday."


Share:

JPM Awaapisha viongozi aliowateua katika ikulu ya Chamwino Dodoma






 Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi John Simbachawene kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya.Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Phaustine Kasike kuwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.









 Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Generali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020.

















 Viongozi walioapishwa na Rais, Dkt. John Pombe Magufuli wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kuanzia kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Dkt. Delphine Magere-RAS Pwani, Jacob Kingu-Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Balozi Phaustine Kasike Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Balozi John Simbachawene Balozi wa Tanzania nchini Kenya pamoja na Brigedia General John Mbungo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.










Rais, Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Viongozi mbalimbali aliowaapisha Wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma leo tarehe 21 Mei 2020. PICHA NA IKULU


Share:

Kumbukumbu la Blogu

ZA HIVI KARIBUNI