Mbunge wa jimbo la Mbulu nchini Tanzania ameelezea wasiwasi wake kuhusu vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kupumua vinavyotokea kwa wingi katika jimbo lake, Gazeti la Mwananchi limeripoti.
Katika kikao cha bunge mjini Dodoma, bwana Zacharia Isaay ameitaka Serikali ya Tanzania kueleza kina sababu inayopelekea watu kufa kwa ugonjwa unaofanana, ambao huwa wanaita 'pneumonia', matatizo ya kupumua
"Serikali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika,"amesema Isaay.
Mbunge huyo ameelezea wasiwasi wake katika msimu huu wa baridi jimboni labda hali inaweza kuwa mbaya zaidi.
"Jana nilikwenda hospitali ya hapa Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa,watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi lakini nimesema," Mwananchi imemnukuu mbunge huyo.
Aidha, Mbunge huyo ameomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha dawa za miti shamba ambazo ameeleza kuwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa lakini akabainisha kuwa zinapatikana kwa gharama kubwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni