Mamlaka ya utangazaji ya China imelipiga marufuku shirika la utangazaji la Uingereza BBC kurusha matangazo yake nchini humo, ikilituhumu kwa kukiuka miongozi, kufuatia ripoti yenye utata kuhusu nama nchi hiyo inavyowatendea watu wa jamii ya wachache ya Uinghur. Uamuzi huo umekuja siku chache tu baada ya mamlaka ya mawasiliano ya Uingereza kufuta leseni ya shirika la utangazaji la CGTN kwa kukiuka sheria ya Uingereza kuhusu umiliki unaoungwa mkono na serikali, na kusababisha shutuma za hasira kutoka London. Hatua hiyo inazidi kuyaweka pabaya mahusiano katika nchi hizo mbili, ambayo yametiwa doa na hatua ya China kuanzisha sheria ya ya usalama katika koloni la zamani la Uingereza la Hong Kong. Uingereza pia imelipiga marufuku shirika la teknolojia ya mawasiliano la China Huawei kutoshiriki katika mfumo wa mawasiliano wa G5, baada ya Marekani kuelezea wasiwasi kwamba shirika hilo linatumiwa na serikali ya China kuzifanyia uchunguzi nchi nyingine. Katika tangazo la usiku, mamlaka ya usimamizi wa redio na Televisheni ya China (NRTA), imesema report za BBC World News kuhusu China zilibainika kukiuka vibaya miongozo ya utangazaji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni