Benki ya biashara Tanzania (TCB) yafunguliwa rasmi
Waziri wa fedha na mipango,mheshimiwa Mwigulu Nchemba amefungua rasmi benki ya Taifa ya biashara (TCB),ambayo ni muunganiko wa benki mbili nchini, TIB na TPB ikiwa na shabaha ya kuundwa kwa benki kuu ya biashara ya serikali yenye ushindani katika soko ikitoa huduma za kibenki na biashara.
Akitoa maelezo hayo wakati wa uzindizi wa benki hiyo,waziri huyo amesema kwamba benki hizo zimeunganishwa kisheria,hivyo wafanyakazi wa benki hiyo wanapaswa kujituma na kuwa na ubunifu katika kutimiza majukumu yao ya kikazi sambamba na kuenda na malengo na maono ya benki hiyo.
Pia waziri huyo ameongeza kwa kusema kuwa wateja wote waliokuwa katika benki mbili za mwanzo wataendelea kuhudumiwa na benki hiyo ya TCB kwa uweledi wa halii ya juu.
Mwisho waziri Mwigulu nchemba amewaasa taasisi za mabenki kupaunguza riba kwa wateja wao,ikiwa pamoja na kuangalia jinsi wanavyofilisi mali za wateja wao,pindi wanaposhindwa kurudisha mikopo yao.
Afrika Kusini- Idadi ya waliofariki kwenye vurugu yafikia 212
Idadi ya waliofariki kutokana na ghasia ambazo zinaendelea nchini Afrika ya kusini imefikia 212,kutoka vile 117 vilivyoripotiwa hap awali.
Waziri wa nchi,ofisi ya rais nchini umo,Khumbudzo Ntshavheni amesema kwamba vifo vilivyoongezeka vimetokea jimbo la kwa zulu-natal,ambapo ndipo kwenye kiini cha machafuko hayo kwa sasa.
Hadi sasa watu zaidi ya 2,500 wameshakamatwa kutokana na vurugu hizo zilizokaa karibu wiki nzima,zikiambatana na uchomaji wa majumba ya biashara na uporaji.
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ameahidi kuwafatilia wale waliopanga njama ili kuanzisha vurugu hizo. Kwa sasa utulivu umeanza kurejea nchini humo.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo March 31, 2021
Ni siku nyingine njema, kutoka Dar es salaam leo March 31, 2021,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania.




















Kampuni ya Nike yawasilisha kesi kwa madai ya kuhusishwa na Viatu vyashetani

Kampuni ya Nike inashitaki ubunifu wa kampuni ya MSCHF iliyopo Brooklyn juu ya uzinduzi wa kile kinachosemekana kuwa "Kiatu cha shetani" chenye tone la damu ya kweli ya binadamu kwenye soli za viatu.
Viatu hivyo vinavyouzwa kwa dola 1,018 sawa na (pauni 740), ambavyo vimechorwa alama ya msalaba iliyopinduliwa na pentagramu (nyota ya ncha tano katika duara) na maneno "Luka 10:18", vimetengenezwa kwa kuboresha muundo wa kiatu cha Nike Air Max 97s.
Kampuni ya MSCHF ilitoa jozi ya viatu 666 Jumatatu ikishirikiana na mwanamuziki Lil Nas X na kusema kwamba vyote viliuzwa chini ya dakika moja.
Kampuni ya Nike imedai kuingiliwa kwa chapa au alama ya biashara ya kampuni yake.
Viatu vya rangi nyeusi na nyekundu "vilivyotolewa" na kampuni ya MSCHF Jumatatu, kulikwenda sambamba na uzinduzi wa nyimbo mpya ya mwanamuzi Lil Nas X ya Montero ya (Call Me By Your Name), ambayo ilitolewa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube Ijumaa iliyopita.
Katika video ya muziki huo, mwanamuziki huyo wa rapa anateleza kwenye mlingoti kutoka peponi au mbinguni hadi jehanamu au motoni, akiwa amevaa viatu hivyo.
Taswira na hiyo na viatu ambavyo vimeandikwa andiko la Bibilia Luka 10:18 - "Akawaambia, 'Nilimuona shetani akianguka kama radi kutoka mbinguni'."
Kila kiatu kina soli maalum ya muundo wa kampuni ya Nike yenye sentimita za ujazo 60 za wino mwekundu na tone la damu ya binadamu, ambayo ilichangiwa na wanachama wa kampuni hiyo.
Kampuni ya Nike ambayo ni maarufu kwa viatu vya michezo imesema kuwa katika kesi yake iliyowasilishwa kwenye mahakama moja mjini New York, kuwa haiidhinishi au kuruhusu utengenezaji wa 'Viatu vya Shetani'.

Kampuni ya Nike inataka mahakama kusitisha kampuni ya MSCHF kuuza viatu hivyo na pia kuwazuia kutumia nembo yao ya muda mrefu maarufu kama 'Swoosh'.
"Kampuni ya MSCHF na viatu vyake vya shetani ambavyo havijaidhinishwa kuna uwezekano mkubwa kukasababisha mkanganyiko na dhana fulani na kutengeneza fikra mbaya kati ya bidhaa ya kampuni ya MSCHF na kampuni ya Nike," Kampuni hiyo ya utengenezaji viatu vya michezo imesema katika kesi yake iliyowasilisha.
"Kwanza, tayari kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha mkanganyiko na dhana potofu sokoni, ikiwemo simu zinazotaka watu kususia bidhaa za kampuni ya Nike kufuatia uzinduzi wa viatu vya shetani vya kampuni ya MSCHF, ambavyo inaonekana kana kwamba kampuni ya Nike ndiyo ambayo imeidhinisha na kuruhusu utengenezaji wa bidhaa za hiyo."
Kesi iliyowasilishwa inarejelea ujumbe wa mtandao wa Twitter uliotumwa na mshawishi mkubwa wa viatu @Saint Ijumaa iliyopita, ambao ulianza kuarifu wateja wake kuhusu kuzinduliwa kwa viatu hivyo na kuvipa umaarufu zaidi kwa umma wikendi kwenye mtandao wa kijamii na hata vyombo vya habari vya Marekani.
Baadhi ya wenye msimamo mkali akiwemo gavana wa Dakota Kusini Kristi Noem, na wafuasi wengine wa kidini, wameshutumu viatu hivyo vyenye utata na kumkosoa rapa Lil Nas X na kamupuni ya MSCHF kwenye mtandao wa Twitter.
Hata hivyo, Lil Nas X alimjibu gavana huyo pamoja na viongozi wa kidini kwenye mtandao wa Twitter, na Jumatatu katika mtandao huo, kulikuwa na vibonzo vya mzaha kwenye wasifu wake baada ya kampuni ya Nike kusema kwamba imechukua hatua ya kisheria.
Philip Mpango apendekezwa kuwa Makamu wa Rais Tanzania
Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Philip Isdory Mpango kuwa makamo wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jina hilo liliwasilishwa bungeni asubuhi ya Jumanne na mpambe wa rais katika bahasha maalum.Baada ya kupokea Spika Job Ndugai alilitangazia bunge hilo jina hilo lililopendekezwa na Rais Samia.Mara baada ya tangazo hilo bunge lililipuka kwa shangwe.Bwana Mpango amekuwa waziri mwandamizi katika serikali ya hayati John Magufuli akihudumu kama waziri wa fedha.Kwa sasa, bunge la Tanzania linatarajiwa kupiga kura ili kuthibitisha uteuzi huo wa Mpango.Na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania, asilimia 50 ya wabunge wanatakiwa kuukubali uteuzi huo ili kuthibitishwa.
Kabla ya jina hilo kuwasilishwa bungeni hii leo, kwanza liliwasilishwa katika Kamati kuu ya chama tawala CCM na kuthibitishwa.
'Nimepigwa na butwaa'
Mara tu baada ya jina lake kusomwa Spika Ndugai alimpatia Mpango muda wa kujieleza ndani ya Bunge.
Mpango akaeleza kuwa hakujua chochote juu ya uteuzi huo na kwamba alipigwa na butwaa.
'...Hii ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota (kama nitaipata)...Mpaka Naibu Waziri wangu akiwa anajibu maswali asubuhi hapa, nilikuwa nafikiria majukumu yangu yanayonikabili ikiwemo mishahara ya wabunge ambayo baadhi imechelewa mpaka asubuhi hii. Nimepigwa na butwaa..."
Phillip Mpango ni nani?

Dkt. Philip Mpango amekua Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano, ameteuliwa katika baraza la mwanzo la mawaziri la Rais John Magufuli.
Mwaka 2015 Alikua mbunge wa kuteuliwa.
Bwana Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu.
Dkt. Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi - Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.
Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi.
Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alikuwa akifundisha "Microeconomics", "Macroeconomics" (kwa mwaka wa pili) na "Public Finance" kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili. (Kwa tafsiri yangu, Uchumi mdogo, Uchumi mkubwa na masuala ya Fedha za umma.)
Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais.
Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.
JPM alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.
Katika uchaguzi wa mwaka 2020 alishinda kiti Cha ubunge jimbo la Buhingwe.
Kisha kuteuliwa tena kuwa waziri wa fedha na Mipango.