Benki ya biashara Tanzania (TCB) yafunguliwa rasmi
Waziri wa fedha na mipango,mheshimiwa Mwigulu Nchemba amefungua rasmi benki ya Taifa ya biashara (TCB),ambayo ni muunganiko wa benki mbili nchini, TIB na TPB ikiwa na shabaha ya kuundwa kwa benki kuu ya biashara ya serikali yenye ushindani katika soko ikitoa huduma za kibenki na biashara.
Akitoa maelezo hayo wakati wa uzindizi wa benki hiyo,waziri huyo amesema kwamba benki hizo zimeunganishwa kisheria,hivyo wafanyakazi wa benki hiyo wanapaswa kujituma na kuwa na ubunifu katika kutimiza majukumu yao ya kikazi sambamba na kuenda na malengo na maono ya benki hiyo.
Pia waziri huyo ameongeza kwa kusema kuwa wateja wote waliokuwa katika benki mbili za mwanzo wataendelea kuhudumiwa na benki hiyo ya TCB kwa uweledi wa halii ya juu.
Mwisho waziri Mwigulu nchemba amewaasa taasisi za mabenki kupaunguza riba kwa wateja wao,ikiwa pamoja na kuangalia jinsi wanavyofilisi mali za wateja wao,pindi wanaposhindwa kurudisha mikopo yao.
Afrika Kusini- Idadi ya waliofariki kwenye vurugu yafikia 212
Idadi ya waliofariki kutokana na ghasia ambazo zinaendelea nchini Afrika ya kusini imefikia 212,kutoka vile 117 vilivyoripotiwa hap awali.
Waziri wa nchi,ofisi ya rais nchini umo,Khumbudzo Ntshavheni amesema kwamba vifo vilivyoongezeka vimetokea jimbo la kwa zulu-natal,ambapo ndipo kwenye kiini cha machafuko hayo kwa sasa.
Hadi sasa watu zaidi ya 2,500 wameshakamatwa kutokana na vurugu hizo zilizokaa karibu wiki nzima,zikiambatana na uchomaji wa majumba ya biashara na uporaji.
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ameahidi kuwafatilia wale waliopanga njama ili kuanzisha vurugu hizo. Kwa sasa utulivu umeanza kurejea nchini humo.